HAKIELIMU
About UsAbout Us About Us Events Current Features Publication Friends of education Links Contact
Publications Publications Publications
Publications Publications Publications
 
 
 

Je ni rahisi kwako kupata taarifa kuhusu namna fedha zinavyotumiwa shuleni?
Ndiyo
Hapana
Sijui

 



 
 

Dira ya HakiElimu ni kuona kuwa kila mtoto wa Tanzania anapata haki yake ya kupatiwa elimu bora ya msingi katika shule zinazojali na kuheshimu utu, kukuza ubunifu na kuwawezesha wanafunzi kujifunza bila woga kwa kuuliza maswali, kutoa changamoto na kutafakari kwa kina na kuinua haki za binadamu na demokrasia.

Sisi HakiElimu tunaamini kuwa elimu nchini Tanzania itaimarika na kuboreshwa zaidi iwapo sote tutashiriki kikamilifu. Kwa sababu hiyo hatujaribu kutatua matatizo mengi sisi wenyewe, bali tunatafuta na kutoa nafasi na fursa kwa wananchi wenyewe kutatua matatizo hayo wao wenyewe!

Tovuti hii itakupatia taarifa zaidi kuhusu Dira ,Dhamira malengo, mikakati na programu zetu pamoja na historia yetu. Inajumuisha pia uchambuzi wetu wa hali ya elimu nchini Tanzania na kukuunganisha na nyaraka nyingine muhimu. (Bonyeza hapa ili kuweza kupata kipeperushi kinachoelezea kwa ufupi shughuli zetu kikiwa katika mfumo wa zip file). Tovuti hii itakupa mwanga kuhusu HakiElimu na muktadha/mazingira ya kazi yetu, hata hivyo iwapo utakuwa na maswali zaidi, tafadhali usisite kuwasiliana nasi.

Aidha, tungependa kufahamu kuhusu wewe, mawazo na dukuduku zako kuhusu elimu nchini Tanzania! Tafadhali piga kura yako ya maoni au toa maoni yako katika sehemu maalumu hapo pembeni au wasiliana nasi. Tutachangia maoni yako na watu wengine ikiwa ni pamoja na wale wanaofanya maamuzi. Tuandikie na utusaidie kuleta mabadiliko katika elimu nchini Tanzania.

 
 
Tarehe Tukio
Jul 2008 Zaidi hapa
Jan 2008 Shule Nzuri ni Ipi? Zaidi hapa
Jan 2008 Miaka Miwili ya Utawala wa Serikali ya Awamu ya nne.Je Serikali inatimiza ahadi zake Zaidi hapa
Oct 2007 Je,Elimu ya Sekondari Inaendelea?Taarifa za Muhimu kutoka katika Mapitio ya Serikali ya utekelezaji wa MMES Zaidi hapa
Oct 2007 Mafanikio gani ymefikiwa Elimu ya Msingi? Zaidi hapa
 
 
 

 

HakiElimu © 2002-2007